TDS yachachafya michuano ya Iber
Timu ya wasichana chini ya miaka 14 ya programu ya kuendeleza vipaji (TDS) imekuwa na mwendelezo mzuri katika michuano ya Kombe la Iber inayoendelea nchini Ureno baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya klabu ya New York Soccer.
Huu ni ushindi wa tatu mfululizo kwa tTDS katika michuano hiyo baada ya kushinda mechi mbili dhidi ya Women Soccer School A’ na Women Soccer School B’, zote kutoka nchini Hispania.
TDS itacheza mechi ys mwisho hatua ya makundi leo Julai 03, 2026 dhidi ya timu ya Pa Team Academy ya Hispania saa 10 jioni. Endapo TDS itashinda mechi hiuo itatinga hatua ya nusu fainali.
Lengo la michuano ya Iber ni kutoa nafasi kwa wachezaji kucheza mechi za ushindani kimataifa, kukuza vipaji vya wachezaji wachanga, kuunganisha Dunia kupitia mpira wa mihuu, lakini pia ni nafasi nzuri ya makocha na mawakala kutazama, kutathimini na kufuatilia vipaji vya wachezaji ili kuwapa fursa mpya.
Michuano ya Iber ilianza Juni 25 na itamalizika Julai 5, 2026 ambapo zaidi ya timu 400 kutoka nchi mbalimbali zinashiriki michuano hiyo.


