Fainali Kombe la CRDB kuchezwa Pemba

    Mechi ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Benki ya CRDB (CRDB Federation Cup) itachezwa tarehe 4 Julai 2026.

    Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba ndiyo utakuwa mwenyeji wa mechi hiyo kati ya timu za Simba na Azam za Dar es Salaam itakayofanyika kuanzia saa 11.00 jioni.

    Fainali hiyo ndiyo itakayohitimisha mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa msimu wa 2025/2026.

    Timu hizo zimefuzu kucheza fainali baada ya kushinda mechi zao za nusu fainali. Simba iliitoa Coastal Union wakati Azam iliing’oa Yanga ambayo ilikuwa inatetea Kombe hilo.

    Share.