Tanzania makamu bingwa CECAFA U-17

    Timu ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 17 (Serengeti Girls) imeshika nafasi ya pili katika michuano ya CECAFA 2026 huku Uganda ikitwaa ubingwa wa michuano hiyo iliyomalizaika Juni 23 katika Uwanja wa KMC, Dar es Salaam.

    Serengeti Girls imemaliza katika nafasi hiyo baada ya kupoteza mechi ya fainali dhidi ya Uganda kwa mabao 3-0.

    Uganda imeibuka bingwa wa michuano hiyo ikiweka rekodi ya kushinda mechi zote na kutoruhusu bao lolote.

    Mabao ya Uganda yalifungwa na Justine Ayerango dakika ya 38, Brendah Nassaka (42), na Flavia Yagala (48).

    Tuzo mbalimbali zilitolewa baada ya fainali ambapo kipa bora ni Namuhaya Mayimuna wa Uganda, wakati Mchezaji bora ni Shadia Nabirye pia wa Uganda. Tuzo ya mfungaji bora ikichukuliwa na Bahati Kizanguzi wa Tanzania.

    Tuzo zingine ni timu yenye nidhamu (Sudan Kusini), na tuzo ya mshindi wa tatu iliyochukuliwa na Kenya.

    Michuano ya CECAFA U-17 ilianza Juni 13, 2026 ikijumuisha timu nane kutoka Kanda ya CECAFA.

    Share.