Nyota 23 wameitwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) kwa ajili ya mechi mbili za kufuzu Olimpiki dhidi ya Botswana.

    Kikosi hicho kinachotarajia kuingia kambini Oktoba 1, 2026 chini ya Kocha Bakari Shime kinajumuisha nyota wanane wanaocheza nje ya Tanzania.

    Wachezaji hao ni Najiath Abbas (JKT Queens), Nusra Hamis (Fountain Gate), Janeth Shija (Simba Queens), Anastazia Katunzi (JKT Queens), Julitha Singano (Al nassr, Saudi Arabia), Ester Maseke (JKT Queens), Vaileth Nicholaus (Simba Queens), Enekia Lunyamila (Gallos Femenil, Mexico) na Diana Mnally (Yanga Princess).

    Wengine ni Noela Luhala (MFA Zalgiris, Lithuania), Fatuma Issa (Simba Queens), Winfrida Castor (JKT Queens), Elizabeth Chenge (JKT Queens), Diana Msewa (Trabzonspor, Uturuki), Hasnath Ubamba (Madrid Cff, Hispania), Elizabeth Joseph (Simba Queens), na Mary Siyame (Simba Queens).

    Wengine ni Clara Luvanga (Washington Spirit, Marekani), Aisha Masaka (Brighton, Uingereza), Bahati Steven (JKT Queens), Aisha Mnunka (Simba Queens), Opah Clement (Alula Club, Saudi Arabia) na Asha Rashid (JKT Queens).

    Twiga Stars inatarajia kuanzia ugenini Botswana na kumalizia nyumbani.

    Share.