Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza kampeni za kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) 2027 ikipoteza kwa mabao 2-0 dhidi ya Guinea Bissau.
Mchezo huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Amaan Complex, Zanzibar kwa miamba hiyo kusaka tiketi ya kucheza fainali hizo zitakazofanyika kwa pamoja katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda.

Pamoja na Taifa Stars kutawala mchezo kwa muda wote waliruhusu bao katika kipindi cha kwanza, kabla Guinea Bissau kuongeza bao la pili katika kipindi cha pili.
Mchezo wa pili wa Stars utakuwa dhidi ya Madagascar utakaochezwa Septemba 29, 2026 nchini Morocco kabla ya kucheza michezo miwili ya kirafiki itakayochezwa nchini Morocco.

Taifa Stars ambayo imeshafuzu kucheza fainali hizo kutokana na kuwa mmoja ya wenyeji, ipo kundi L pamoja na Guinea Bissau, Madagascar na Nigeria.


