Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) imeanza kukusanya alama kwenye michezo ya kufuzu AFCON 2027 baada ya kutoka sare ya bao 1-1 na Madagascar ugenini.

    Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Stade d’Honneur de Maknes uliopo katika mji wa Meknes nchini Morocco, Taifa Stars ndiyo walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 39 kupitia kwa Cyprian Kachwele.

    Bao la Taifa Stars ilidumu hadi mapumziko kabla ya Madagascar kusawazisha katika kipindi cha pili dakika ya 50 kwa bao lililofungwa na Nicolas Fontaine.

    Mchezo unaofuata wa Taifa Stars utakuwa dhidi ya Nigeria utakaochezwa Novemba 11, 2026 wakiwa ugenini, kabla ya kurudiana nao Novemba 15, 2026 wakiwa nyumbani.

    Share.