Timu ya Taifa ya Tanzania U17 (Serengeti Boys) imekaa kileleni mwa msimamo wa michuano ya Kombe la Vertex baada ya raundi ya kwanza ya michuano hiyo.
Serengeti Boys imekaa kileleni ikiwa na alama tatu na bao moja la kushinda kufuatia ushindi wake wa bao 1-0 dhidi ya China wakati nafasi ya pili ikichukuliwa na Argentina yenye alama 1, nafasi ya tatu ikishikiliwa na Mexico ambao pia wana alama 1 huku China wakiburuza mkia wakiwa hawajavuna alama yoyote.
Mchezo unaofuata wa Serengeti Boys utakuwa dhidi ya Argentina utakaochezwa Oktoba 4, 2026, kabla ya kumalizana na Mexico katika mchezo wa mwisho utakaopigwa Oktoba 7, 2026.


