Fainali ya Ngao ya Jamii ya Wanawake itakayowakutanisha wababe wa Ligi ya Wanawake (WPL) Simba Queens na JKT Queens unatajwa kama mchezo wa kisasi wanapokutana.

    Mchezo huo utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa KMC, Mwenge jijini Dar es Salaam utakuwa marudio ya fainali ya 2025 ambayo JKT iliibuka na ushindi wa mabao 2-1.

    Kocha wa Simba Queens, Mussa Mgosi amesema msimu huu wamejipanga kulipa kisasi kutoka kwa wapinzani wao baada ya kupoteza katika fainali ya msimu uliopita, hivyo kesho wamejipanga kwa ushindi.

    Kocha wa JKT Queens, Kessy Juma

    Kocha wa JKT Queens, Kessy Juma, amesema mchezo wa fainali dhidi ya Simba utakuwa mgumu lakini wamejipanga kuhakikisha wanatetea Ngao waliyoibeba msimu uliopita.

    Kabla ya mchezo huo kutakuwa na mchezo wa kutafuta mshindi wa tatu ambao utazikutanisha timu za Yanga Princess dhidi ya Mashujaa Queens, huku kiła timu ikitamba kuibuka na ushindi.

    Share.