Timu ya Taifa ya Tanzania ya Wavulana U15 imepangwa Kundi X katika fainali za Kombe la Dunia zinazotarajiwa kuanza Oktoba 21 mpaka 30, 2026 nchini Azerbaijan.

    Katika Kundi hilo Tanzania imepangwa na Zambia, Uruguay, Comoros, Moldova na Montenegro.

    Mchezo wa kwanza wa Tanzania utachezwa Oktoba 24, 2026 dhidi ya Zambia na Oktoba 25 watakuwa na michezo miwili dhidi ya Comoros ukifuatiwa na mchezo dhidi ya Montenegro.

    Tanzania itamaliza hatua ya makundi Oktoba 26, 2026 kwa michezo miwili dhidi ya Uruguay na Moldova.

    Share.