Timu ya Simba Queens imeibuka Bingwa wa Ngao ya Jamii Wanawake baada ya kuichapa JKT Queens kwa bao 1-0 katika mchezo uliochezwa leo Oktoba 3, 2026, kwenye Uwanja wa KMC Complex jijini Dar es Salaam.
Bao pekee la Simba Queens kaaika mchezo huo lilifungwa kipindi cha pili dakika ya 62 na mchezaji Aisha Mnunka.
Hata hivyo kabla ya mchezo huo ulishuhudiwa mchezo wa mshindi wa tatu ambao pia ulitamalizika kwa Yanga Princess kupata ushindi wa mikwaju ya penati 5-4, baada ya kumalizika kwa sare ya bao 1-1 katika dakika 90.
Ikumbukwe michezo yote hiyo ya Ngao ya Jamii rasmi imefungua Ligi Kuu ya Wanawake msimu 2026/27.


