Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania U23, Hamad Ally amesema wachezaji wake wamepambana lakini bahati haikuwa yao wameshindwa kusonga hatua inayofuata ya kufuzu AFCON 2027
Hamad ametoa kauli hiyo baada ya ya kikosi chake kushinda dhidi ya Kenya kwa mabao 3-1, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ushindi ambao haukuweza kupindua matokeo ya awali wakipotreza mabao 4-1 mchezo uliochezwa Nairobi.
Mabao ya Tanzania katika mchezo huo yalifungwa na Sheikhan Khamis na Seleman Mwalimu aliyefunga mabao mawili.
Akizungumza baada ya mchezo, Kocha Hamad alisema licha ya kutolewa kwenye hatua hiyo lakini amefurahishwa na kiwango walichoonesha wachezaji wake.
Alisema wachezaji wake walionesha uwezo mkubwa wa kupambana, sambamba na kufuata maelekezo ukilinganisha na namna walivyocheza kwenye mchezo wa awali ugenini.
“Haikuwa bahati tumeshindwa kufuzu lakini morali ilikuwa ni kubwa, mipango na wachezaji walifuata maelekezo katika malengo tuliyojiwekea. Hivyo nimefurahi na najivunia nyakati nyingi nillzopanga tuzifanye uwanjani ziliweza kufanyika kama tulivyotaka,” alisema Hamad.
Alisema pamoja ya maelekezo hayo lakini kwa bahati mbaya kwao ni kuruhusu bao ambalo limewapa nafasi Kenya ya kusonga.


