Timu ya Taifa ya wavulana U15 imewasili katika mji wa Baku nchini Azerbaijan kwenye Tamasha na Kombe la Dunia litakaloanza Oktoba 24 hadi 30, 2026.

    Kocha wa kikosi hicho, Mohamed Amin amesema kikosi kimewasili salama na programu inayofuata ni kupata muda wa kupumzika na kujiandaa na mchezo wa kwanza dhidi ya Zambia.

    Tanzania imepangwa Kundi X katika tamasha hilo ikiwa na timu za Zambia, Uruguay, Comoros, Moldova na Montenegro.

    Mchezo wa kwanza wa Tanzania utachezwa Oktoba 24, 2026 dhidi ya Zambia na Oktoba 25 watakuwa na michezo miwili dhidi ya Comoros ukifuatiwa na mchezo dhidi ya Montenegro.

    Tanzania itamaliza hatua ya makundi Oktoba 26, 2026 kwa michezo miwili dhidi ya Uruguay na Moldova.

    Share.