Timu ya Taifa ya Wavulana U15 imetembeza kichapo kwa Montenegro na Comoros katika mechi mbili za Kombe la Dunia zilizochezwa leo Baku nchini Azerbaijan.

    Katika mechi ya kwanza iliyocheza asubuhi Tanzania ilicheza na Comoros na kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.

    Mabao ya Tanzania yalifungwa na Seleman Deus aliyefunga mawili, wakati Sule Msuya na Jerryson Simon wakifunga bao moja kila mmoja.

    Katika mechi ya pili iliyochezwa jioni, Tanzania iliwatandika Montenegro kwa mabao 6-1.

    Bao la kwanza la Tanzania lilipatikana kwa Montenegro kujifunga, huku mengine yakifungwa na Jerryson Simon, Is-haka Twaha, Selemani Deus, Abdikadil Simba na Frank Chacha.

    Tanzania imepangwa Kundi X katika tamasha hilo ikiwa na timu za Zambia, Uruguay, Comoros, Moldova na Montenegro.

    Share.