Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Miguel Gamondi amesema kikosi chake kina wachezaji wengi wazuri wanaoweza kushinda dhidi ya Uganda katika mechi yao ya pili ya Kundi C kwenye Fainali za Kombe la Afrika (AFCON).Miguel ameyasema hayo katika mkutano na wanahabari kwa ajili ya mechi hiyo itakayochezwa Jumamosi, Desemba 27 Uwanja wa Al Medina, jijini Rabat saa mbili na nusu usiku.”Hii ni dabi na itakuwa mechi ngumu, lakini ubora wa wachezaji na mbinu ndizo zitakazoamua mechi. Tuna wachezaji wazuri wanaoweza kuamua mechi kama Msuva, Samatta na wengine. Lakini pia uwepo wa Feisal katika mchezo huu utaongeza nguvu ya kikosi kufanya vizuri,” alisema Gamondi.Naye Simon Msuva akizungumza kwa niaba ya wachezaji alisema: “Tunawaheshimu Uganda lakini tunataka ushindi na hatuna chaguo lingine zaidi ya ushindi. Hii si mara ya kwanza kucheza na Uganda, tumeshacheza nao mechi nyingi na bila shaka kesho tutawafunga”.Timu zote mbili zitaingia katika mechi hiyo zikiwa hazina pointi yoyote baada ya kupoteza katika mechi zao za kwanza. Tanzania ilipoteza dhidi ya Nigeria kwa mabao 2-1 na Uganda ikipoteza dhidi ya Tunisia mabao 3-1.Ends …
Wednesday, September 30
Trending
BUY TICKETS
- Taifa Stars kujipima na Morocco
- Taifa Stars yaanza kukusanya alama AFCON
- Timu zatambiana Ngao ya jamii wanawake 2026
- Tanzania kujipanga upya nyumbani
- TFF yatangaza Katibu Mkuu mpya
- Taifa Stars yaanza kampeni AFCON 2027
- Ngorongoro Heroes yahamishia nguvu Kombe la Dunia
- 23 waitwa Twiga Stars kuwavaa Watswana Olimpiki


