Simba yaongeza taji lingine

     

    Timu ya Simba ndiyo mabingwa wa michuano ya Kombe la Shirikisho la benki ya CRDB (CRDB Bank Federation Cup) msimu wa 2025/2026.

     

    Bao la kujifunga la Yahya Zayd wa Azam FC ndilo lililofanya Simba iibuke na ushindi katika mechi ya fainali iliyofanyika leo tarehe 4 Julai kwenye Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba.

     

    Zayd alijifunga dakika ya 61 wakati akijaribu kuzuia mpira wa adhabu uliopigwa na mchezaji Ellie Mpanzu wa Simba.

     

    Azam ilicheza pungufu katika muda mwingi wa fainali hiyo baada ya Mwamuzi Sifu Amon kutoka Mbeya kumtoa kwa kadi nyekundu mchezaji wao wa tegemeo Feisal Salum.

     

    Hilo litakuwa taji la pili msimu huu kwa timu ya Simba yenye maskani yake Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam baada ya kutwaa Kombe la Muungano.

     

    Fainali hiyo ndiyo iliyohitimisha mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa msimu wa 2025/2026.

    Share.