TDS yashinda mashindano Ureno

    Timu ya wasichana chini ya miaka 14 ya programu ya kuendeleza vipaji (TDS) imetwaa ubingwa wa michuano ya Iber baada ya kuifunga Golden Soccer ya Hispania bao 1-0 katika mechi ya fainali.

    TDS ilifuzu kucheza fainali baada ya kuifunga timu ya PA Academy Hispania bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa tarehe 3 Julai katika uwanja wa Maristas, Ureno.

    Bao la Anjelina James dakika ya 46 liliipa timu ya TDS ubingwa na kuweka rekodi ya kumaliza michuano pasipo kupoteza mchezo wowote.

    TDS imemaliza michuano ya Iber ikiwa imefunga jumla ya mabao 21 na kuruhusu bao moja pekee katika mechi sita ilizocheza katika michuano hiyo.

    Michuano ya Iber itamalizika tarehe 5 Julai ambapo tuzo mbalimbali zitatolewa kwa timu zilizofanya vizuri. Huu ni msimu wa 17 kwa michuano hii kufanyika tangu ilipoanzishwa mwaka 2009 nchini Ureno.

    Share.