What's Hot

    Timu ya Taifa ya Wanaume U23 inayoisaka tiketi ya kucheza fainali za AFCON 2027 imelazimika kupiga hesabu upya kuwakabili Kenya kwenye mchezo wa marudiano, utakaochezwa Oktoba 6, 2026.

    Hatua hiyo imekuja baada ya kupoteza kwenye mchezo wa Raundi ya kwanza ugenini kwa magoli 4-1 Septemba 28, 2026.

    Kwa matokeo hayo Tanzania inahitaji ushindi wa kuanzia mabao matatu huku ikilazimika kutoruhusu bao katika mchezo wa nyumbani ili kujihakikishia kusonga mbele.

    Timu hiyo inatarajia kucheza mchezo wa marudiano kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, ikifanikiwa kuwaondosha Kenya, watakutana na Ivory Coast.

    Share.