Yanga bingwa tena NBC
Ligi Kuu ya NBC imetamatika tarehe 30 Juni 2026 kwa timu ya Yanga kutangazwa tena kuwa mabingwa baada ya kufikisha pointi 72.
Yanga imehitimisha Ligi hiyo kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji JKT Tanzania katika mechi iliyofanyika Uwanja wa Meja Jenerali Isamuhyo, Dar es Salaam.
Hilo ni taji la tano mfululizo kwa Yanga ikirejea historia yake ya msimu wa kuanzia mwaka 1968 hadi 1972.
Timu nyingine iliyotwaa taji hilo mara tano mfululizo ni Simba SC. Simba ilitwaa taji hilo kuanzia mwaka 1976 hadi 1980.
Simba SC iliyomaliza katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 70 pamoja na Yanga zitacheza Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2026/2027.
Azam FC iliyoshika nafasi ya tatu, na Singida Black Stars SC iliyomaliza namba nne zitaiwakilisha Tanzanka michuano ya Kombe la Shirikisho barani Afrika.
KMC ya Dar es Salaam na Mtibwa Sugar ya Manungu, Morogoro zimeshuka daraja ambapo msimu wa 2026/2027 zitacheza Ligi ya Championship ya NBC.


