Timu ya Futsal yaingia kambini
Timu ya taifa ya wanaume ya Futsal imeingia kambini leo Julai 7, 2026 katika hoteli ya Chichi, Da es Salaam kujiandaa na mechi mbili za kirafiki dhidi ya Zambia.
Mechi hizo za kirafiki zitachezwa tarehe 19 na 21 Julai nchini Zambia katika Uwanja wa ndani wa Automotive.
Mechi hizo pia zitatumika kama sehemu ya maandalizi ya fainali za AFCON zitakazofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Tanzania ilifuzu kushiriki fainali za Kombe la mataifa Afrika (AFCON) kwa upande wa futsal baada ya kuiondosha Ivory Coast katika mechi ya mwisho wa kufuzu kwa jumla ya mabao 9-7 chini ya Kocha Curtis Reid.

Wachezaji walioitwa ni David Gasper, Hansgally Gasto, Mshenga Salim, Derick Charles, Awadh Salum, Jamal Saleh, Ahmed Shaha, Ramadhani Mshaghasho na Athumani Iddy.

Wengine ni Sharif Khamis, Gidio Paul, Ally Kipekepeke, Laurent Haji, Tariki Mohamed, Nkwabi Joseph, Bashir Salum na Habeel Moshi.


