Twiga Stars yatolewa WAFCON

    Timu ya Taifa ya Wanawake (Twiga Stars) imekamilisha mechi tatu za hatua ya makundi ya michuano y WAFCON na kupata pointi tatu pekee.

    Ilishinda mechi dhidi ya Afrika Kusini (Banyana Banyana) na kupoteza nyingine mbili.

    Akizungumza baada ya mechi ya mwisho dhidi ya Ivory Coast iliyochezwa Agosti 3, jijini Casablanca, Morocco na kumalizika kwa Twiga Stars kupoteza kwa mabao 2-1, Kocha Mkuu wa timu hiyo Bakari Shime alisema:

    “Tumechukuwa mechi zote kama somo ili kurudi kujipanga kuhakikisha tunarejea tena kwenye Fainali hizi. Lengo letu lilikuwa kufika hatua za mbele zaidi kama nusu fainali.”

    Alisema nahodha wake Opah Clement hakuwa vizuri kwenye utimamu wa mwili, hali iliyosababisha timu kurudi nyuma kwa kiasi kikubwa hasa kwenye safu ya ushambuliaji.

    Timu tano tayari zimefuzu kucheza hatua ya robo fainali ya michuano hiyo. Timu hizo ni Afrika Kusini, Algeria, Cameroon, Ivory Coast, na wenyeji Morocco.

    Share.