Shime: Tumejifunza kwa Brazil

    Kocha wa timu ya Taifa ya Wanawake U20 (Tanzanite Queens), Bakari Shime amesema mechi ya kwanza dhidi ya Brazil, Fainali za Kombe la Dunia imekuwa somo kwake kwa ajili ya mechi zijazo.

    Shime ametoa kauli hiyo kufuatia matokea ya kupoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya Brazil, mechi iliyochezwa Uwanja wa Bielsko-Biala, Septemba 5, 2026.

    Bao pekee la Tanzania (Tanzanite Queens) lilifungwa na Winfrida Gerald kipindi cha kwanza, kabla Brazi hawajafanya mabadiliko kipindi cha pili yaliyobadili taswira ya mechi kwa Tanzanite na kuruhusu mabao zaidi.

    Hata hivyo, Tanzanite bado ina mechi mbili kwenye hatua ya makundi, ambapo inayofuata ni dhidi ya England kabla ya kumalizana na Canada.

    Mechi hizo ndiyo zitakazoamua kama Tanzania itacheza hatua ya 16 bora.

    Share.