Timu ya Taifa ya wanaume U20 (Ngorongoro Heroes) imefanikiwa kukata tiketi ya kucheza Fainali za AFCON 2027 kwa Kanda ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA), zitakazofanyika nchini Ghana.

    Ngorongoro Heroes imefuzu baada ya kuichapa Burundi mabao 2-0 na kuwa moja kati ya timu mbili zitakazowakilisha Ukanda wa CECAFA katika fainali hizo ya AFCON 2027.

    Mabao muhimu ya Ngorongoro Heroes dhidi ya Burundi yalifungwa na Juma Abushiri dakika ya 17 na Faraji Kayanda dakika ya 33.

    Ngorongoro Heroes itashuka tena dimbani katika mchezo wa fainali dhidi ya Sudan, utakaochezwa Septemba 24, 2026 huku ikisaka rekodi yake ya kumaliza michuano hiyo bila kuruhusu nyavu zake kutikiswa.

    Kabla ya mchezo wa nusu fainali dhidi ya Burundi, Ngorongoro Heroes ilianza kwa kuichapa Rwanda kwa mabao 3-0 na kuitandika Ethiopia mabao 4-0.

    Fainali za AFCON 2027 ni mara ya tatu mfululizo kwa Ngorongoro Heroes kufuzu.

    Share.