Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajia kujipima nguvu na Timu ya Taifa ya Morocco katika mchezo wa kirafiki utakaochezwa Oktoba 5, 2026.

    Taifa Stars ambayo ipo nchini Morocco, itatumia kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kucheza michezo miwili ukiwemo dhidi ya Morocco, utakaochezwa katika mji wa Tangier.

    Kabla ya mchezo huo Taifa Stars itacheza mchezo mwingine wa kirafiki Oktoba 2, 2026 utakaochezwa Rabat.

    Share.