Timu ya Taifa ya Tanzania U17 (Serengeti Boys) imeanza kwa kishindo michuano ya Kombe la Vertex baada ya kuichapa China kwa bao 1-0 katika mchezo wa kwanza.

    Bao pekee la Serengeti Boys limefungwa na Luqman Ally dakika ya 83 na kuifanya timu yake kuweka kibindoni pointi tatu huku ikisubiri michezo miwili ya mwisho.

    Serengeti Boys inatumia mashindano hayo yaliyoanza leo Oktoba 1, 2026 na kumalizika Oktoba 7 mwaka huu kama sehemu ya maandalizi ya Kombe la Dunia litakalofanyika nchini Qatar mwezi Novemba mwaka huu.

    Michezo miwili ya Serengeti Boys iliyobaki itavaana na Argentina mchezo utakaochezwa Oktoba 4, 2026 na mwisho itamalizana na Mexico mchezo utakaopigwa Oktoba 7, 2026.

    Share.