Timu ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania (Twiga Stars) imewasili katika jiji la Gaborone kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa kwanza wa kufuzu Olimpiki Los Angeles 2028 dhidi ya Botswana.
Mchezo huo utachezwa Oktoba 9, 2026 mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa Oktoba 13, 2026 jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Twiga Stars imewasili nchini humo ikiwa na wachezaji 22 kati ya 24 huku wachezaji wawili Clara Luvanga na Aisha Masaka wakitarajiwa kuungana na wenzao baada ya majukumu ya kuzitumikia klabu zao


