Timu ya Simba Queens imeendeleza ubabe Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) baada ya kubeba pointi tatu nyingine mbele ya watani wake Yanga Princess kwenye mchezo uliomalizika kwa ushindi wa mabao 2-0.Mechi hiyo iliyochezwa Desemba 28, 2024 Azam Complex Chamazi, Dar es Salaam ulivutia washabiki wengi kwa kasi yake huku timu zote zikionesha dhamira ya kushinda.Hata hivyo uongozi wa mechi ulianza kutwaliwa na Simba Queens waliotumia uzoefu wao vizuri kuwasumbua walinzi wa Yanga Princess na kufanikiwa kuandika bao la kwanza dakika ya 36 kupitia mshambuliaji wao Jentrix Shikangwa.Kipindi cha pili timu zote zilirejea na kasi ileile, wakati Yanga Princess ikitafuta bao la kusawazisha, Simba Queens waliendelea kuimarisha ulinzi hadi walipoongeza bao la pili.Kwa matokeo hayo Simba Queens imefanikiwa kupanda kileleni na kuongoza ligi ikiwa ndio timu pekee ambayo haijadondosha alama yoyote hadi raundi hiyo, ikifikisha pointi 15.Matokeo ya mechi nyingine ni; Geita Queens 3-1 Ruangwa Queens, Tausi FC 1-2 Alliance Girls, Bunda Queens 1-1 Ceassia Queens, Bilo 0-3 Fountain Gate Princess na JKT Queens 6-0 Mashujaa Queens.Ends…
Thursday, November 26
Trending
BUY TICKETS
- Tiketi ya Serengeti Boys ipo kwa Ireland
- Serengeti Boys yaanza kwa sare Kombe la Dunia
- Kiswahili sasa lugha rasmi ya CAF
- Simba Queens yabanwa, JKT yatakata TWPL
- Gamondi afurahishwa kiwango cha Taifa Stars
- Yanga Princess yaibamiza Kilimanjaro Wonders
- Kiwango cha Ngorongoro Heroes chamridhisha kocha
- Kamungo, Starkie waongeza nguvu Taifa Stars


