Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premium Lager, leo imepoteza mchezo wake wa kwanza kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017 baada ya kufungwa kwa mabao 3 - 0 na wenyeji Misri.

Taifa Stars ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na hasa sehemu ya ulinzi ilifanya kazi ya ziada kuokoa mashambulizi ya washambuliaji wa timu ya Misri, na kupelekea kwenda mapumziko -0 - 0.

Msafara wa timu ya Taifa ya Tanzania (taifa Stars) inayodhaminiwa na kampuni ya bia ya Kilimanjaro Premium Lager tayari umewasili salama katika eneo la Borg El Arab jijini Alexandria na kufikia katika hoteli ya Panacea tayari kwa mchezo wake wa kesho.

Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini nchini Ethiopia kwa takribani wiki moja, iliondoka jana usiku Addis Ababa  na kuwasili uwanja wa ndege wa Cairo majira ya saa 8 usiku, kisha kuunganisha kwa usafiri wa basi mpaka Borg El Arab takribani masaa matatu.

Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula kesho jumamosi atafunga rasmi mashindano ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 13.

Sherehe ya kufunga mashindano hayo itafanyika katika uwanja wa CCM Kirumba kuanzia majira ya saa9 kamili alasiri.

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro Premier Lager, leo siku ya ijumaa jioni inatarajiwa kuondoka Addis Ababa Ethiopia kuelekea nchini Misri tayari kwa mchezo wa siku ya jumapili.

Stars ambayo imeweka kambi ya mazoezi takribani kwa wiki moja sasa jijini Addis Ababa leo imeendelea na ratiba yake ya mazoezi katika uwanja wa Taifa, ambapo jana imefanya mazoezi yake asubuhi tu.

Uongozi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo umekutana na Uongozi wa klabu ya Simba  SC ukiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Collin Frisch na mchezaji Ramadhani Yahya Singano akiandamana na Uongozi wa Chama cha Wacheaji wa Mpira wa Miguu (SPUTANZA). Kikao hiki kiliitishwa na TFF kujadili utata wa kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.

Katika kikao cha leo pande zote zimeeleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.